0


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro anawatangazia wanchi wote wenye sifa zilizoainishwa hapo chini kutuma maombi ya kazi kama ifuatavyo

KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III NAFASI 1

SIFA ZA MUOMBAJI;
Wenye elimu ya kidato cha nne (IV), waliomaliza mafunzo ya uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika Programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.

KAZI MAJUKUMU YA KUFANVA
i.    Kuchapa barua, taarifa na nyarakaza kawaida
ii.    Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanayoweza kushughulikiwa.
iii.    Kusaidia kutunza kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitaji   
iv.    Kusaidia kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
v. Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake w akazi kwa wasidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
vi.    Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa waliokatika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
vii.    Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi

MSHAHARA
Ngazi Ya Mshahara Wa Serikali Yaani TGS B.

2. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 2

SIFA ZA KUINGILIA
Kuajiriwa mwenye cheti cha  mtihani wa kidato cha 4 au 6 wenye leseni ya daraja c ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila  ksababisha ajali

KAZI ZA KUFANYA
- kuendesha magari ya abiria namaroli
- Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri na usafi wakati wote na kufanya Uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo.
- Kufanya matengenezo madogomadogo katika gari.
- Kutunza na kuandika daftari la Safari “Log – book” kwa Safari zote.
- kufanya matengenezo madogo madogo katika gari

Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV), wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali, wenye cheti cha Majaribio ya Ufundi daraja la II.

umri kati ya miaka 18 - 40

  MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara vya serikali yaani TGOS  A 

3.  MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 87

KAZI ZA KUFANYA
-Kusimamia ulinzi na Usalama wa raia na mali zao.
-Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
-Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
- kusimamia mapato na matumizi ya Serikali ya Kijiji

 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
Awe amehitimu elimu ya kidato cha Sita/Nne na Mafunzo ya Astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma, au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA
Ngazi Ya Mshahara Wa Serikali Yaani TGS B. 
 
MASHARTI YA JUMLA 
i/ mwombaji awe raia wa Tanzania na awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote ya Halmashuri ya Wilaya ya Morogoro
ii/ mwobaji awe na umri usiozidi miaka 45 na awe hajawahi kupatikana na kosa lolote la jinai kufungwa jela au kufukuzwa katika utumishi wa umma
iii/ waombaji waambatanishe maelezo binafsi
iv/ maombi yote yaambatanishwe na nakala za vyeti vya taaluma, vyeti vya kidato cha 4 cheti cha kuzaliwa na picha 2 za rangi za hivi karibuni na ziandikwe jina nyuma
v/ waombaji walosoma nje ya tazania wakahakikishe vyeti vyao  TCU NA NACTE na taarifa za uhakiki iambatanishwe  kwenye maombi
vi/ watakao wasilisha vyeti na sifa za kughushi watchukuliwa hatua za kisheria

mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 8/10/2017

maombi yote yatumwe kwa 
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA MOROGORO,
S.L.P 1880,
MOROGORO

Post a Comment

 
Top